Pages

Sunday, September 14, 2008

SHUKRANI PIA KWA WASAIDIAO KITUO HIKI CHA MAKALALA (ITALY).

Hii ni siku tulipo kutana kwa chakula cha jioni hapa Cesena-Italy, kwaajili ya kusaidia kituo cha watoto yatima Makalala-Mafinga-Iringa. Ilikuwa mwezi wa nne mwaka huu ambapo watu wengi walijitokeza kuchangia, kituo hiki kinaendeshwa kwa kutegemea misaada ya watu wa kawida wala si matajili, mara kwa mara watu hukutana kwenye chakula, kama hapa chakula kilikuwa euro 15 kwa kila mtu, na wakaamua kuweka iwe euro 30 ili 15 zingine ziende kituoni Makalala. Hata sisi Tanzania tunaweza kufanya hivi, kwa kile kidogo tulicho nacho tunaweza kusaidia sana watoto wetu wanao hangaika bila kuwa na msaada wowote. Pia mimi nilipata nafasi ya kutoa shukrani zangu za dhati kwa niaba Tanzania kama Mtanzania. Nilifurahishwa sana na jambo hili, pia niliwasomea methali na hadidhi mbalimbali kwa kiswahili na kutafsiri, kama zawadi yangu kwao.
Pia kikundi cha Band ndogo ya Cesena kilitumbwiza kufurahisha watu, kama mchango wao kwa Makalala.


Mimi na Mtanzania mwenzangu alipo kuja kwa mda hapa Cesena kikazi, pia yeye akitokea huko Makalala.


Wa kwanza ni Rogger mgeni kutoka Tanzania, wa pili ni dada Malaika mwanzilishi wa kituo cha Makalala, wa tatu ni mimi mwenyewe, wa nne Ivani mdau mkubwa wa Makalala, wa tano Rafaeli mdau mkubwa wa Makalala. Siku hiyo ya kuwa pamoja kwaajili ya Makalala.




Watu kwa pamoja nguvu moja kwa Makalala, hapa Cesena mwezi wa nne mwaka huu.


0 idadi ya maoni: