Monday, September 15, 2008
KIKAO CHA MAKALALA- CESENA.
Jioni hii tunakutanika vijana mbalimbali wa hapa Cesena, kujadili mambo mbalimbali ya kituo cha watoto yatima Makalala. Pia mimi nita simulia likizo yangu niliyo ifanyia huko Makalala mwezi wa nane mwaka huu. Pia tutajadili swala la kukutana tena kwa chakula cha jioni ili kuchangia kituo hiki. Ni nia moja ya kukutana, kukaa pamoja, kubadilishana mawazo, lengo hasa kusaidia. Maana kituo hiki kinategemea misaada kupitia kwa watu, hakina shirika lolote kama vituo vingine, huwa tunakutana kama hivi kwenye chakula na viburudisho mbalimbali, lakini lengo hasa ni kusaidia hawa watoto yatima, ambao kweli wanahitaji misaada kutoka kwetu sote.
0 idadi ya maoni:
Post a Comment