Pages

Thursday, November 12, 2009

MTOTO ATUMBUKIA SHIMONI NA KUFA HUKO MOROGORO.








Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Malipula eneo la Chamwino mkoani Morogoro, wakiangua vilio vyao baada ya kuwaona wafanyakazi wa kikosi cha zimamoto wakiopoa maiti ya mtoto HAWA(1.5) aliyetumbukia juzi jumanne majira ya saa moja usiku katika shimo lililochimbwa jirani ya nyumba kwa lengo la kujenga choo. Wananchi wa mtaa huo waliofurika katika eneo la tukio wakijipanga barabarani kwa uchungu na kuangalia gari la Polisi likiondoka na mwili wa marehemu. Mmiliki wa nyumba yenye shimo hilo, Bw.Azani Ngata anashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo.
-Picha na: DANSTUN SHEKIDELI - MOROGORO.


0 idadi ya maoni: