Pages

Monday, September 28, 2009

NIMEPATA E-MAIL YA MDAU:KWA KUTOA SHUKRANI ZAKE ZA PEKEE KWA DAVIDE NA MARA.

E-MAIL YA MDAU INASEMA HIVI:

Kutoka katika sakafu ya moyo wangu, naomba kutuma salamu zangu na pongezi kubwa kwa Bwana Davide na Mara, katika sherehe ya ndoa yao iliyofanyika Agosti 15, 2009.

Pongezi hizi zimekuja kutokana na moyo wao, kukataa chereko chereko na kuamua michango ya Euro 4000, iwasaidie watoto yatima wa Makalala Children's Home.

Hakuna sentensi ya kuonyesha hisia zangu za shukrani zaidi ya kusema Asanteni sana. Nawatakia maisha mema katika ndoa yao na kuwakaribisha sana waendelee kutembelea Tanzania, na kuhamasisha usaidizi kwa wenye uhitaji, kuliko kuwekeza kwenye minuso. Asanteni sana!

Wasalaam na Shukrani;
Ray Ephraim Ndewingiya Njau.
Dar es salaam, Tanzania.


-Baraka: Nami nasema asante sana Ray Ephraim kwa kuwapongeza hawa jamaa, na nimewafikishia salamu zako, na wote walio washukuru kwa moyo wa dhati hawa jamaa. Wamefurahi sana tena sana kwa mioyo yetu kwa kuwashukuru na kuonyesha upendo.

Pia watu wengi waliniomba contact zangu na zakituo huko Makalala.
Kituoni: Makalala Children's Home, yupo mhusika dada Malaika anaishi huko huko Makalala.

Namba ya simu ya dada Malaika ni: 0754-675001.

Mimi ni: +39/380-3115382. Italy.
E-mail: baraka500@yahoo.co.uk

0 idadi ya maoni: