Pages

Friday, September 25, 2009

HARUSI YA RAFIKI YANGU MPENDWA DAVIDE CAPPONCELLI=IL MATRIMONIO DI UN CARISSIMO AMICO DAVIDE CAPPONCELLI.

1). SPOSI = MAHARUSI.
2). INVITATI = WAALIKWA.

3). AMICI = MARAFIKI.


4). TESTIMONI = WASIMAMIZI.




5). MAKALALA CHILDREN'S HOME.
Cappo kama aitwavyo, ni rafiki yangu mpendwa sana wa hapa mji niishio Cesena. Mnamo tarehe 15/08/2009, alifunga ndoa na mtarajiwa wake Mara Tani, ila kwa bahati mbaya sikuweza kuhudhulia harusi yao, maana nilikuwa nyumbani Tanzania kwa likizo. Kitu kilicho nifurahisha sana moyoni katika sherehe ya ndoa hii ni; kwamba harusi yao hawa marafiki, imechangia kituo cha Makalala Children's Home kwa Euro 4000 = Shilingi milioni 7, za kitanzania. Hawakuhitaji zawadi kutoka kwa wanandugu na marafiki zao, waliwaomba wasitoe zawadi kwao, bali zawadi zao zote wazielekeze kwa kuchangia kituo cha watoto yatima cha Makalala.
-Mimi mtanzania kwa niaba ya Tanzania kwa ujumla, natoa shukrani zangu nyingi sana kwa hawa wapendwa sana Cappo na Mara, kwa kupata wazo zuri kama hili la kusaidia watoto hawa wanao hitaji msaada, kwa kutumia sherehe yao mhimu ya ndoa.
Ni mfano mzuri sana wa kuingwa kwa jambo zuri kama hili walilo fanya.
Asanteni sana MARA na DAVIDE ( CAPPO ).
= Cappo come lo chiamano in tanti, un mio carissimo amico della città dove vivo a Cesena. Il 15/08/2009, si è sposato con Mara Tani, al Castello di Sorrivoli. Peccato che non ero presente perchè ero a casa in Tanzania. Una cosa grande che mi ha fatto un piacere nel mio cuore è; Cappo e Mara per loro matrimonio hanno datto 4000 Euro per il centro di Makalala Children's Home. Hanno voluto dare questo regalo tramite i loro amici chiedendo di non fare a loro regali invece di fare a questi bambini Tanzaniani che hanno bisogno. Una cosa bellissima, sono molto contento.
-Io dico come tanzaniano è per tutta la Tanzania, grazie grazie mille Cappo e Mara per questo bel regalo che avete fatto per questi bambini tanzaniani bisognosi, del mio paese. Un grande esempio a tutti noi da seguire.
ASANTENI SANA DAVIDE CAPPONCELLI NA MARA TANI!
-Baraka.




4 idadi ya maoni:

Anonymous said...

nawapongeza sana Bwana Cappo na Bi Mara kwa mchangowao wa hali na mali kufanikisha kupatikana kiasi hicho cha pesa kwakweli nimfano mzuri sana wa kuigwa. kitendo chao chakuifanya harusi yao kuwa harambee hakika sijambo dogo ktk dunia hii ya sasa, ikizingatiwa imejaa mijisifa na mijigambo ktk jamii yetu, big up brother.

Mikingamo said...

Salamu,
Kuna picha moja nieona umepiga na Don. Sebastiano wa Precious blood
Mnafahamiana na huyu Padre na yuko wapi kwa sasa. ni mlezi wangu kule Itigi na Dodoma

ella said...

tunaweza kupata information au no za simu ili tuweze kuwasiliana na nayi kama tuna chochote cha kuwapa.

Anonymous said...

CHIBIRITI EBU TUPE HISTORIA YAKO PENGINE INAWEZA KUTUSAIDIA WENGINE NASI TUKAPATA ELIMU NA MAWAZO YA KUSAIDIA WATU KAMA WEWE, I MEAN THAT COULD ME A FORWARD PUSH FOR US TO DO AS YOU DO, YOU COULD BE A ROLE MODEL FOR OTHERS MAN!!! WE NEED YOUR PROFILE.