Kweli usemi huu ni wamaana sana na ni wakweli kabisa, wiki iliyopita nilitembelea huko mji wa Birmingham-England-UK, na nilifanikiwa kukutana na mdau na mpenzi mkubwa wa Fotobaraza na Blog hii ya Makalala, ambaye ni mama Malaika na familia yake.
Ilikuwa ni furaha sana kukutana na kufahamiana ana kwa ana. Kweli Fotobaraza ni kitu cha maana sana na ni mhimu sana kwetu sisi, maana inatuunganisha sana waTanzania wengi na kuwa kama ndugu kabisa. Hongera sana mwanzirishi wa Fotobaraza (BABUKADJA) na wanakijiji wote wa Fotobaraza Duniani kote kwa ukarimu wenu wa kufahamiana na wa kuitumia vizuri Fotobaraza. Tuzidi sana na sana kudumisha upendo mwingi wa kupendana, kufahamiana na kutembeleana.
0 idadi ya maoni:
Post a Comment