Pages

Thursday, February 5, 2009

MAISHA YA SHULE JINSI YALIVYO MAGUMU TANZANIA=LA VITA SCOLASTICA COME IN TANZANIA.





























Nakumbuka sana maisha haya ya shule, tabu zake na raha zake. Kama nilivyo yaishi mimi na wengine wengi Tanzania. Ilikuwa lazima uwe na:
1). Jembe begani, kwaajili ya: shughuli za kulima shamba la shule na kuweka mazingira safi ya shule ( yaani kulima majani yanayo izunguka shule).
2). Mkononi lazima kuwa na kidumu cha maji, kwaajili ya: kumwagilia mauwa yanayo izunguka shule.
3). Mfuko wa madaftali mgongoni, kwaajili ya: Elimu.
4). Ufagio mkononi, kwaajili ya: kusafisha shule.
5). Kuamka mapema alfajiri saa 12, ili kuwahi namba (kuhesabiwa) ukiwa mchelewaji adhabu inakungoja.
6). Lazima kukimbia daima ili kuwahi shuleni kutokana na umbali uliopo, kutoka nyumbani hadi shuleni.
7). Kukimbia mchaka mchaka kabla ya kuingia darasani, sababu ili kuwa mkakamavu kujenga mwili, hata kama tayari umesha kimbia vyakutosha, kutoka nyumbani hadi shuleni, lakini kwa walimu ilikuwa haitoshi.
8). Ukikosa ni adhabu, na adhabu zanyewe mara nyingi ni viboko, ili siku nyingine usikosee, kuwa na waga wa viboko.
9). Kuwa mwenye upendo kwa wanafunzi wenzako, hata kama ni adui zako, la sivyo kiboko kitakuandama, na kusoma kwa bidii..
10). Michezo mbalimbali: kuimba, kukimbia, kuruka kwa kamba, kucheza mpira na sanaa mbalimbali.
Haya ndo maisha ya shule ya msingi niliyo yapitia mimi na wengine wengi Tanzania.
Maisha ya shule si mchezo Tanzania.
Pamoja na haya yote magumu, sheria ngumu, adhabu, lakini kwa wanafunzi ( kwa vijana) ilikuwa kwao ni funzisho zuri katika maisha, mimi binafsi mambo mengi sana yamenisaidia katika haya maisha.
KIITALY:
Mi ricordo bene come era la vita scolastica in Tanzania, come tutti dovevano comportasi, queste sono alcune regole:
1). La zappa in spalla, per zappare la terra della scuola (pulizia di erba che stava intorno alla scuola).
2). Bisogna avere un secchio di acqua in mano, per annaffiare i fiori che stavano intorno alla scuola.
3).Un zaino dientro alla schena, per i quaderni e libri.
4). La scopa in mano, per pulire la scuola.
5).Bisogna alzarsi mattina presto, alle sei devi essere a scuola, sè no punizione se non riesci ad arrivare in tempo a scuola.
6). Bisogna correre sempre per arrivare in tempo, per le distanze che ci sono da casa a scuola.
7). La ginnastica della scuola si corre cantando, dicevano per tenere il fisico bene: secondo gli insegnante non basta la corsa da casa a scuola, che per me era tantissimo, bisognava correre ancora a scuola.
8). Se sbagli qualcosa o non arrivi in tempo a scuola, la punizione! spesso era due o tre frustata forte con la frusta grande.
9). Bisogna avvere l'amore immenso verso gli altri studenti, anche se qualcuno era tuo nemico, bisognava amare lo stesso, sè no ti frustavano. Poi bisogno mettere molto impegni negli studi, sè no ti frustavano.
10). Tanti tipi di giocchi: correre, saltare, giocare il pallone, cantare e invenzione di tante cose tradizionale.
Questa è la vita scolastica, scuola elementare in Tanzania.
La vita scolastica in Tanzania non è per niente faccile.
Comunque nonostante le regole rigide, l'esperienza della scuola è utile per la formazione del carattere dei ragazzi, e per me è stata una bella esperienza per la mia vita.
-Baraka.






0 idadi ya maoni: