Pages

Saturday, September 27, 2008

FURAHA SANA KWA WATOTO WETU WAKUAPO VIZURI NA KUPATA MAHITAJI YOTE, HASA KWENDA SHULE.

Ni furaha sana kwa wazazi watoto wakuapo vizuri hasa wapatapo mahitaji yote, ya kiafya na kwenda shule ipasavyo n.k. Hata kwa watu wote hata wasio wazazi, ukiona mtoto anapendeza sana ni furaha sana tena sana kwetu sote. Tufanyeje kutokomeza watoto wa mitaani ambao wanahangaika sana kweli ni huruma sana kwa Taifa hili la kesho, ambapo kwakweli wanatia sana huruma, hata sisi watanzania tuanze tabia ya kusaidia watoto wa mitaani, tuone kama ni wa kwetu kabisa na kuwasaidia ipasavyo. Mimi nafurahi sana tena sana kuona watoto wakipendeza vizuri, mahali popote nionapo watoto wenye afya nzuri moyo wangu unafarijika sana.
Filipo rafiki yangu alipo jitolea kwenda kusaidia watoto yatima mwaka 2006, kwa shughuli mbalimbali za kituoni hapo Makalala-Mafinga, ikiwa pia na kuwalea watoto hao kushinda nao. Tunakaribishwa sana Makalala wote.




Hiki kikosi nilicho enda nacho mwaka 2006, kwa kusaidia kazi mbalimbali za watoto yatima Makalala.



1 idadi ya maoni:

Justine said...

Habari! Jina langu ni Justine. Mimi ni Mmarekani, lakini ninakaa Irina mpaka Disemba. Ninajifunza Kiswahili kila asubuhi, na ninataka kuvolontiya mchana na jioni kila siku. Kama utaweza kunisaidia, tafadhali andika: justine.amos@gmail.com.

Asante Sana!