Pages

Wednesday, September 24, 2008

CHAKULA CHA JIONI KWAAJILI YA KITUO CHA WATOTO YATIMA MAKALALA, KIMEENDA VIZURI.

Nipo na Giuditta, dada mwandaaji wachakula na kualika marafiki mbalimbali ili kuchangia kituo cha watoto yatima Makalala.
Mimi na Giuditta, alipo kuwa akihudumia watu kwa chakula.


Dada Giuditta na Mama yake Malaika kwa pembeni, siku ya kujiandaa na kwa chakula hiki. Pia huyu msichana Giuditta anataragia kwenda huko Makalala wiki ijayo, kusaidia kazi mbalimbali za kituoni hapo. Pongezi nyingi sana kwako Giuditta na shukrani sana kwa moyo wako wa kusaidia kituo hiki.


Marafiki zangu wa karibu pia hawakukosa kwenye tukio hili. Mbele kabisa Davide a.k.a Cappo, Ilenia na Anna.










Huyu Dada Cinzia mwenye mimba, ambae anatarajia kujifungua mda si mrefu, hakupenda kabisa kukosa kufika. Nae ni mmoja wa waanzilishi wa Kituo cha watoto yatima Makalala, alianza pamoja na Malaika hadi mambo ya ujenzi alikuwepo huko Makalala baada ya ujenzi kuisha alirudi hapa Cesena, lakini bado ni mmoja wa msimamizi wa kituo hiki kwa huku Italy. Nami namtakia kila laheri katika kujifungua kwake, na kumshukuru sana kwa yote.











Kikundi cha muziki kidogo cha hapa Cesena T.N.T nacho kimetoa mchango wao kuwaburudisha watu na kuvuta watu ili wachangie Makalala.





Vijana mbalimbali mezani kuchangia Makalala.










Pia maongezi kidogo kupata hali halisi ya Makalala, kutoka kwa vijana walio kuwa huko Makalala mda si mrefu wamerudi hapa Cesena.




















Marafiki mbalimbali akiwemo dada wa miwani Natasha rafiki yangu nilimshawishi kwa shida mpaka akakubali kuja, asante sana.









Kikundi kamili, wote hawa walikuwa huko Makalala kusaidia kazi mbalimbali hasa za kupekechua mahindi wakati huu, wamerudi hapa jumamosi iliyo pita, pia mimi nilikutana nao huko Makalala na niliwaacha huko. Asanteni sana kwa moyo wenu wa upendo kwa watoto wetu yatima wa Makalala.











0 idadi ya maoni: