Pages

Thursday, March 10, 2011

SIKU TULIPO TEMBELEA SHULE YA MSINGI TEGETA - DAR.





























































































Siku tulipo tembelea shule ya msingi Tegeta, pamoja na wageni wangu kutoka Italy, Septemba 2010. Ni shule ambayo ipo nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, barabara iendayo Bagamoyo. Shule hii pia anafundisha mama yangu mzazi, yeye pamoja na mwalimu mkuu wa shule hii, walituambia kuwa; ni shule yenye watoto wengi sana bila kuwa na madarasa yakutosha pia madawati ya kukalia. Kwakweli jambo hili huwa la kusikitisha sana, mambo muhimu kama haya ya shule huwa yanasahaulika sana, hii ni shule ambayo ipo Jijini Dar es salaam je za vijijini itakuwaje kwa hali kama hii? Mimi nakubali kuwa sisi ni maskini katika nchi yetu...lakini si umaskini huu wakukosa huduma nzuri katika mashule yetu. Ukichukulia Tegeta kuna shule mbili tu! kweli zinatushinda kuziimarisha vizuri?
Safari bado tunayo ndefu sana tena sana!!!!












0 idadi ya maoni: