Pages

Sunday, April 18, 2010

WATOTO WAWASHUKURU WABUNGE KWA KUWALINDA.




Leo kwa zaidi ya saa moja halaiki ya wanafunzi wapatao 27,127 kutoka maeneo mbalimbali ya Dodoma Mjini, na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, waliandamana kuingia katika uwanja wa Jamhuri - Dodoma kwa kuwashukuru wabunge na Serikali kwa kuwatungia sheria mpya ya watoto inayowalinda.
Maandamano hayo yalipokelewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye alisema yoyote yule atakaye kiuka haki za watoto sasa kuona Wrath ya Serikali, awe mzazi, mlezi au Jamii kwa ujumla. Katika Tamasha hili ambapo watoto waliomba haki zao za watoto ziingizwe katika katiba, kwasababu mpaka sasa kulikuwa hakuna katiba hiyo.
Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa dini kuombea Taifa hili kuachana na mambo ya uuaji wa watoto, ama kwa hakika alisisitiza sana wananchi katika jambo hili kuelewa sheria hiyo mpya ambayo ni kali sana na inayolenga kuweka maisha ya watoto katika hali ya usalama, uadilifu na ubora zaidi.
Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akikagua kazi za mikono za watoto wa kituo cha mlimwa Anglican kabla ya kuhutubia katika Tamasha hilo la kulipongeza Bunge na Serikali. Na pia watoto wakiingia uwanjani wakiwa na mabango yao.
-ASANTENI SANA WABUNGE NA SERIKALI KWA KUWEKA SHERIA KALI KWA WATOTO ILI IWALINDE VYEMA, KWANI WATOTO NI TAIFA LETU LA KESHO LAZIMA WAHESHIMIKE SANA NA KUTUNZWA IPASAVYO.


0 idadi ya maoni: