Pages

Monday, March 28, 2011

RAIS KIKWETE AELEZA KUKERWA NA WATOTO WA MITAANI.

Rais Dk.Jakaya Kikwete, akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto, wakati wa ziara yake ya kikazi Wizarani hapo leo mchana. Katika mkutano wake ameitaka Wizara hiyo kuangalia namna ya kuondokana na tatizo la watoto wa mitaani, ambalo kimsingi linawezekana kabisa kuondolewa hasa kwa kuona baadhi yao wana wazazi wanawatuma kuomba wenyewe wakiwa pembeni. Aidha alitaka juhudi za kukomesha ukeketaji kuendelea. Naye Waziri wa Wizara hiyo Bi. Sophia Simba (unayemwona kulia mwa Rais) alimtaka Rais kusaidia Maofisa Maendeleo Jamii kuajiriwa ili kusukuma mbele maendeleo ya maeneo kama sehemu ya kuepuka ombaomba. SOURCE: Freddy Maro.

0 idadi ya maoni: