Pages

Monday, May 24, 2010

KULEA NI KAZI SANA KAMA HUJAZOEA SI JAMBO DOGO KABISA.

Jamaa yangu Reggi hapo pembeni alikuwa akinicheka sana, maana nilikuwa nikimshika tu mtoto analia kweli kweli, lakini yeye akimchukua ananyamaza. Nikagundua kulea si kazi ndogo, lakini nilivyokuwa mdogo nilimlea vizuri mdogo wangu Josephina na nilikuwa najua kulea vizuri, maana mama yangu alikuwa akienda shule kufundisha ananiachia mtoto ambae ni mdogo wangu Josephina na alikuwa anafujo za kila aina, lakini nilikabiliana nae vizuri tu. Kwasasa nimepoteza uzoefu wa kulea watoto, si kazi ndogo kabisa hongereni sana akina mama kwa kazi nzuri ya malezi ya watoto.

No comments:

Post a Comment