Pages

Thursday, December 17, 2009

KUNA USEMI MZURI KAMA HUU, ILA WAKATI MWINGINE SIKUBALIANI NAO, UNAOSEMA; SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI.


Huu usemi ni mzuri sana, samaki mkunje angali mbichi. Ila wakati mwingine hutumika vibaya, kwasababu Wazazi, Walezi, n.k, huutumia kwa kutesa watoto kwa kusema lazima mtoto ajifunze kazi angali mdogo, ndio nakubali kujifunza kazi kwa mtoto, lakini si hivi kama tuonavyo kwenye picha hizi. Watoto hupata mateso sana wala si kujifunza kazi hivi, watoto wanabeba mizingo mikubwa kupita uwezo wao huku ni kujifunza kazi kweli? Mi naona hizi tabia zimepitwa na wakati kabisa, na tuache kuwanyanyasa watoto kwa kisingizio kupitia usemi huu mzuri wenye maana nzuri tu ya kuwafundisha watoto wawe na tabia njema na maadili mema katika maisha, na wala si kwa kuwatumikisha kwa kusema namkunja angali mdogo. Sikatai kabisa watoto wasifanye kazi wala wasijifunze kazi, bali si kuwafanyisha kazi na kubeba mizigo kushinda uwezo wao, na pia wanakuwa kama watumwa wetu. Wazazi, Walezi tuache kabisa tabia hizi za kuwatumikisha watoto wetu eti tunawafundisha, kumbe tunajipatia wafanyakazi. Watoto wanahitaji sana kukua vyema na kupata zaidi maadili mema ya kimaisha.

0 idadi ya maoni: