Pages

Tuesday, December 1, 2009

DECEMBER 1 2009 WORLD AIDS DAY. THE WORLD COMES TOGETHER = SIKU YA UKIMWI DUNIANI.


Disemba 1 ni siku ya ukimwi duniani, tunawatakia kila laheri wagonjwa wote pia na wauguzaji ili waendelee kuwa na moyo mzuri wa kuwauguza vizuri na si kuwanyanyasa wagonjwa hawa. Pia kwa madaktari na wahudumu wote katika gonjwa hili kila laheri ili mfanye kazi sawasawa kwa wagonjwa hawa. Pia kuwa na taadhari ya kuwa mwaminifu na mwenzi hasa kwa vijana wa taifa la kesho. Pia kwa watoto wote walio athirika kila laheri kwa kupata afya njema!
-Kwa mujibu wa shirika la afya Duniani, kuna watu milioni 33.4 wanaoishi duniani hivi sasa wakiwa na virusi vya ukimwi (VVU) au wanaugua ukimwi.
-Kuna watoto 2.1 wanaoishi na VVU au wanaugua ukimwi duniani.
Watu zaidi ya milioni 25 wamekufa kwa ukimwi tangu mwaka 1981.
Tungependa kutuma fikra na sala zetu kwa wote waliofariki kutokana na ugonjwa huu na wale ambao bado wanaishi na ugonjwa huu.

0 idadi ya maoni: