Pages

Tuesday, November 24, 2009

ANUSURIKA KIPIGO BAADA YA KUHISIWA KAIBA MTOTO ALBINO!




Katikati ya wiki iliyopita, kijana mmoja alinusurika kipigo kutoka kwa wananchi kumhisiwa kaiba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ( Albino) kufuatia kijana huyo kubeba mtoto kama nyani vile, na kurandaranda naye katikati ya Mji wa Morogoro kwa kutumia baiskeli. Wananchi waliomshuhudia kijana huyo akiwa na mtoto huyo albino walimtilia mashaka kwamba huenda amemuiba mtoto huyo. Lakini kumbe haikua hivyo, safari yake na mtoto huyo ilikuwa ni kwenda duka la kuuza maji ya jumla, lililopo maeneo ya Juwata katikati ya Mji kasoro Bahari, na kwamba kijana huyo alipohojiwa alisema kwamba huyo mtoto ni mdogo wake na kwamba aliamua kutembeanae '' ( Huyu ni mdogo wangu nimetokanae nyumbani tumekuja hapa kununua maji ya jumla tumetumwa na mama) '' alisema kijana huyo ambaye alikataa kutaja jina lake.
Miongoni mwa wananchi waliomtilia shaka kijana huyo ni pamoja na Bwana Hussein Ismail ambaye alisema kwamba yeye na wenzake wameshawishika kumtilia shaka kutokana na mazingira ya tukio hilo, pia kumwona kama kijana haaminiki.
- Picha na habari na: DANSTAN SHEKIDELE - MOROGORO.


0 idadi ya maoni: