Kweli kabisa bado tupo dunia ya tatu. Katika pitapita zangu huko vijijini Mkoani Singida nilikutana na watoto wanafunzi wa shule mbalimbali, wakijishughulisha kwa mikono na nguvu zao wenyewe kwa kujenga shule zao wenyewe, kwa kazi za ufyatuaji matofali, kuchota maji ya ujenzi, kusomba mchanga....n.k. Kwakweli nilitokwa na machozi kwa masikitiko, pia kwa furaha kuona watoto wadogo kabisa wakiweka bidii zao zote kwa ujenzi huu wa shule. Na niliweza kuongea na baadhi ya watoto hawa, waliniambia ya kwamba wanafuraha sana kwa ujenzi huu, kwani ni kwa manufaa yao na kwa watoto wao hapo baadae kwa kupata elimu nzuri. Baada ya kusikia maneno haya mazuri kutoka kwa watoto hawa, mwili wangu ulinisisimka kwa furaha sana pia kwa huzuni kwa kazi nzito walio kuwa wakiifanya. Hata mimi nimesoma shule ya msingi huko kijijini na kufanya kazi mbalimbali za shule, lakini siwafikii hawa watoto kwa kazi nzito wazifanyazo. Maana shule na nyumba za waalimu tumezikuta zikiwa zimejengwa na serikali. Ujembe kwa serikali ijitahidi zaidi na zaidi kwa ujenzi wa shule vijijini, wasiache watoto wakajijengea wenyewe shule zao badala ya kusoma.
KIITALY:
Veramente ancora siamo nel terzo Mondo. Ho visitato alcuni villaggi nella Regione di Singida-Tanzania, ho incontrato dei bambini studenti delle scuole elementare di varie scuole nei villaggi. Stavano contruendo la scuola con la forza delle loro mani, facendo i mattoni, portavano l'acqua, sabbia è la giaia per la costruzione. Veramente mi sono commosso a vedere come lavorano, mi è venuto anche la tristezza, perchè come si fa a fare lavorare questi piccoli bambini? Quando vedevo questi bambini che ci mettevano tutte le loro forze per costruire la loro scuola mi sono vergognato di tante cose. Poi sono riuscito a parlare con alcuni bambini chiedendo...come mai fate questi lavori? Loro mi hanno risposto dicendo...che sono conteti di costruire la loro scuola perchè è molto utile per loro è anche per loro futuri figli per avere l'educazione migliore. Quando ho sentito queste belle parole da questi bambini, tutto il mio corpo si è commosso di gioia. Poi avevo anche la tristezza, perchè sono ancora piccoli per fare questi lavori. Anch'io ho studiato nella scuola elementare in un villaggio sperduto, facendo tanti lavori duri, però non sono arrivato a questo punto di fare questi lavori per la costruzione della scuola come questi bambini, perchè la scuola è stata costruita dal governo. Spero tanto anche in questi villaggi il governo faccia il suo dovere di costruire le scuole di non lasciare che questi bambini si costruiscano da soli le loro scuole.
-Baraka.
0 idadi ya maoni:
Post a Comment