Pages

Friday, April 24, 2009

KUMBUKUMBU YANGU NINAVYO IKUMBUKA SHULE=IL MIO RICORDO DELLA SCUOLA.



Kwenda shule ni furaha sana kwa watoto, mimi binafsi nakumbuka sana shule hasa shule ya msingi, kutokana na mambo mengi mazuri niliyo jifunza, na hasa yamenisaidia katika haya maisha ninayoishi sasa. Nimeweka hizo picha kukumbuka hasa mchezo wa mpira ambao nilikuwa naupenda sana na kupendwa sana na watoto wenzangu walivyo kuwa wakipenda kuucheza. Na hasa kumbukumbu kubwa ya mwalimu aliyekuwa akitufundisha kucheza, daima alikuwa akisema; Elimu kwanza kabla ya mambo yote, kisha kucheza mpira na mambo mengine yote hufuata. Unaweza kuwa mchezaji mpira mzuri sana lakini kama hujui kusoma na kuandika wengi watakucheka sana na utakuwa mjinga sana katika maisha, hata mpatapo watoto wenu mkumbuke kuwafundisha jambo hili, ndivyo alivyokuwa akisema daima. Elimu ni msingi wa maisha, hivyo watoto wote wanapaswa kwenda shule. Kila lakheri kwa watoto wote.
KIITALY:
Andare a scuola è una gioia per i bambini, il mio ricordo della scuola elementare di tante cose che ho imparato, soprattutto che queste cose mi hanno aiutato tanto per la mia vita. Ho messo queste foto per ricordare un grande maestro di calcio per noi ragazzi, che ci insegnava non solo il calcio, anche come comportaci nella vita. Che ci insegnava dicendo sempre; Studiare per i bambini è più importante di tutte le cose nel Mondo, poi vengono i giochi. Diceva ricordate sempre questo anche quando avrete i vostri figli. Puoi diventare un grande giocatore però sè non sai leggere è scrivere è un problema nella vita, studiare è molto importante è un fondamento nella vita di tutti quanti. Tutti bambini devono riuscire andare a scuola, auguro con il cuore.

0 idadi ya maoni: