Pages

Tuesday, December 30, 2008

SHUKRANI KWA WANA KIJIJI WOTE WA FOTOBARAZA.









Napenda kutoa shukrani zangu za kufunga mwaka huu wa 2008 kwa wana kijiji wote wa Fotobaraza kwa ukarimu wao wote kwa mambo mbalimbali. Pia kwa Mkuu Babukadja kwa kuanzisha jambo zuri kama hili, kwa kutuunganisha pamoja kwa kufahamiana watu mbalimbali na wengine tumekuwa marafiki sana, pia kama ndugu kabisa. Pia Mkuu Michuzi Jr napenda kumshukuru sana kwa ukarimu wake wa kusaidia blog hii ya Makalala Children's bila yeye mambo mengi yasinge kwenda mbele zaidi. Kwa kumaliza mwaka huu basi napenda kuwasalimu sana tena sana wana fotobaraza wote na wapenzi wafuatiliaji wa blog hii ya Makalala Children's home, siwezi kuwataja majina kwasababu ni wengi sana, lakini basi tupo pamoja daima hata kwa mwaka huu ujao wa 2009. Kila lakheri nyingi sana kwa wadau wote!
Ni mimi Chibiriti.

0 idadi ya maoni: