Mwezi wa nane 2009, nilipata nafasi ya kutembelea kituo cha watoto yatima na pia walemavu cha Padri Benzi Oreste, kilichopo Bunju - Dar es salaam. Nilifurahi maana nilibahatika kumfahamu na kukutana nae kwa maongezi kidogo na Padri Benzi, ambaye alikuwa maarufu sana hapa Italy. Alikuwa ni mtu wa watu na kupendwa sana, nilikutana nae huko mji wa Rimini-Italy kabla ya kifo chake, nilimpenda sana kwa mazungumzo yake na pia alivyokuwa hodari kwa mambo mbalimbali mazuri aliyoyafanya hapa duniani wakati wa uhai wake. Alipenda sana kusaidia watoto, vijana na watu wote kwa ujumla wenye shida mbalimbali. Marehemu Padri Benzi ameacha vituo mbalimbali duniani, ambayo vinafanya kazi mbalimali vizuri kwa kusaidia watu wenye shida hasa watoto na vijana. Ametuachia msingi na upendo mwingi kwa mambo mengi mazuri aliyo yafanya hapa duniani.
Don.Benzi ni Padri ambaye alifanya kazi ya Mungu kwa ukweli bila kumwogopa mtu yoyote hapa duniani mwenye kudharau utu wa mtu. Tunakushukuru sana Padri Benzi kwa upendo wako hasa kwa watoto wenye shida mbalimbali hapa duniani.
Na Mwenyezi Mungu azidi kukupumzisha kwa amani daima huko kwake mbinguni, na uzidi kutuombea zaidi ili vituo vyako vyote ulivyo tuachia hapa duniani vizidi zaidi na zaidi kutoa huduma inayostahili katika kusaidia watu wote wenye shida.
KIITALY:
Il mese di Agosto 2009, sono riuscito a visitare il centro per i bambini orfani è handicapatti di Don.Benzi Oreste, che sta a Bunju - Dar es salaam. Ero molto contento di visitare questo centro, perchè tempo fa ho avuto onore di conoscere in persone Don.Benzi, quando ancora era in vita. L'ho incontrato a Rimini, sono riuscito a parlare con lui tante cose belle che faceva per aiutare la gente. Ero rimasto colpito molto per il suo lavoro che facceva per gli altri, dedicando lui stesso. Aiutava veramente chi ha bisogno sopratutto ai bambini, ragazzi è tutta la gente bisognosa.
Mi ricordo la sua semplicità verso tutta la gente, una cosa che mi colpi milto, Don.Benzi un esempio bellissimo da seguire a tutti noi. Don.Benzi ha lasciato molti centri al Mondo per i servizi della gente che veramente hanno bisogno di questi centri. Ha lasciato un fondamento di amore immenso per i bambini, i ragazzi è tutti noi. Don.Benzi ha lavorato senza vergogna, senza paura di nessuno al mondo per difendere i più deboli al Mondo, questa è una cosa molto bella, che personalmente mi colpisce molto nel mio cuore.
Grazie mille (Asante sana) Don.Benzi Oreste per il tuo grande amore verso i bambini, i ragazzi è a tutti quanti, è Dio ti benedica sempre che riposi in pace. E' ricordati sempre di noi nelle tue preghiere che ancora abbiamo bisogno che i tuoi centri che hai lasciato che continuano a funzionare sempre bene ai servizi della gente bisognosa.
-Baraka.
2 idadi ya maoni:
Buona sera vorrei sapere se il centro di Don Benzi si trova a Tegeta in quanto vorrei visitarlo. grazie.
Siiii, si trova a Tegeta.
Post a Comment